YAH: MAHITAJI YANAYOTAKIWA KAMA VIAMBATANISHO ILI KUWEZA KUKAMILIKA KWA UANDAAJI WA HATIMILIKI ZA VIWANJA VILIVYOPIMWA
Kutokana na kuwepo kwa tatizo la wahitaji wengi wa Hatimiliki kutokuwasilisha nyaraka/viambatanisho vinavyotakiwa katika uandaaji wa hatimiliki zao, tatizo ambalo limekuwa mojawapo ya sababu za ucheleweshaji wa hatimiliki zao, ofisi imeamua kuorodhesha hapa chini mahitaji muhimu yanayotakiwa kuwasilishwa kwa waombaji wote wa Hatimiliki za viwanja/mashamba yaliyopimwa.
1.KWA MMILIKI MMOJA MMOJA
i.Barua ya kuomba kumilikishwa kiwanja
ii.Picha sita(6) za passport size
iii.Nakala mbili (2) halisi (Certified Copies) za uthibitisho wa uraia (Kitambulisho cha Uraia/Cheti za Kuzaliwa/Passport ya Kusafiria)
iv.Nakala mbili (2) halisi (Certified Copies) za Uthibitisho wa umiliki wa kiwanja (Mkataba wa kununua kiwanja/Muhtasari wa Halmashauri ya Kijiji au Mtaa)
2.KWA KAMPUNI YA KITANZANIA
i.Barua ya kuomba kumilikishwa kiwanja
ii.Nakala mbili (2) halisi (Certified Copies) za Uthibitisho wa umiliki wa kiwanja (Mkataba wa kununua kiwanja/Muhtasari wa Halmashauri ya Kijiji au Mtaa)
iii.Nakala mbili (2) halisi za Memorandom and Article of Associationya Kampuni
iv.Nakala mbili (2) halisi za Certificate of Incorportionya Kampuni
v.Nakala mbili (2) halisi (Certified Copies) za uthibitisho wa uraia za wakurugenzi wa Kampuni husika (Kitambulisho cha Uraia/Cheti za Kuzaliwa/Passport ya Kusafiria)
3.KWA KAMPUNI ISIYO YA KITANZANIA
i.Barua ya kuomba kumilikishwa kiwanja
ii.Nakala mbili(2) halisi za Certificate of Incentives kutoka TIC
iii.Nakala mbili (2) halisi (Certified Copies) za Uthibitisho wa umiliki wa kiwanja (Mkataba wa kununua kiwanja/Muhtasari wa Halmashauri ya Kijiji au Mtaa)
iv.Nakala mbili (2) halisi za Memorandom and Article of Associationya Kampuni
v.Nakala mbili (2) halisi za Certificate of Incorportionya Kampuni
vi.Nakala mbili (2) halisi (Certified Copies) za uthibitisho wa uraia za wakurugenzi wa Kampuni husika (Kitambulisho cha Uraia/Cheti za Kuzaliwa/Passport ya Kusafiria)
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.