UTARATIBU WA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI
Muombaji wa kibali cha ujenzi anatakiwa kufuata utaratibu ufuatao
1.Barua ya maombi ya kibali cha Ujenzi
2.Picha nne (4) za passport size zinazofanana
3.Nakala nne (4) za michoro ya majenzi (Architectural Drawings na Structural Drawings) na kugongwa muhuri wa Architects.
4.Hati ya kiwanja (Certificate of occupancy) au Mkataba wa Mauziano uliopitishwa katika serikali ya Kijiji na Muhtasari wa Kijiji/Mtaa uliopitisha mauziano hayo.
5.Uthibitisho wa Uraia (Kitambulisho cha Uraia/Cheti cha kuzaliwa/Passport ya kusafiria) ziwe nakala halisi (Certified copy of the Original)
6.Maombi na viambatanisho vyote viwasilishe katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.