Wananchi wa wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wametakiwa kuweka kando utofauti wa vyama vya siasa badala yake wagombee na kupiga kura huku wakiweka mbele amani na tulivu kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa .
Akitoa salamu za serikali mbele ya waumini wa dini ya kiislamu sambamba na wananchi mbali mbali aliowandalia futari ofisini kwake mwishoni mwa wiki Sanga alisema tukio hilo amelifanya ili kuleta ushirikiano .,umoja na mshikamano ndani ya jamii.
Aidha dc Sanga alitumia fursa hiyo kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastic na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mkuranga kuwasimamia watendaji wa vijiji kutenga maeneo maalum ambayo wananchi wanatakiwa kusalimisha kabla ya hatua zaidi za kukabidhi (NEMC).
“Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa hivi karibuni alitoa maagizo mpaka ifikapo june 1 ndio mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastic,hivyo ni marufuku matumizi ya plastic na atakae kamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yake” Alisema Sanga.
Aidha Sanga aliwageukia wafanyabiashara wadogo na watoa huduma wadogo ambao mauzo ghafi yao hayazidi sh 4milioni kwa mwaka wahakikishe wananua vitambulisho na kuvivaa ili kuepukana na mkono wa sheria hapo baadaye.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya siasa Wilaya Ally Msikamo pamoja na kumpongeza Mkuu huyo kwa kuwa kutanisha wananchi kupitia futari aliwataka wapiga kura kuwapima wagombea wenye maslahi binafsi kwa sababu wanatisha kama ukoma.
Akimsomea dua Mkuu wa Wilaya akisaidiwa na waumini wengine Sheikh Mkuu wa Wilaya Almasi Mzee alimpongeza Sanga huku akimnukuu Mtume Muhamad( swa) aliyasema mtoaji zaidi kuliko wengine apewe heshima kuliko wengine na kuweka bayana watafurahi akipanga zaidi nafasi yake aliyonayo kwani bado wanamuhitaji.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.