Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Filberto Sanga amewataka watendaji vijiji na kata sambamba na wenyeviti wa vjiji kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji mapato ya ndani kwenye maeneo yao ili kuirahisishia serikali kutekeleza miradi ya maendeleo sekta mbali mbali
Akizungumza kwenye kikao kazi leo Sanga aliyekua Mwenyekiti wa kikao aliwafafanulia wajumbe kuwasuala hilo la muhimu mno kipindi hiki ambacho nchi imeingia kwenye uchumi wa kati na kusababisha baadhi ya Nchi Wahisani kufuta misaada.
Mkuu huyo ambaye alikua Makao Makuu ya Nchi Dodoma kupata maelekezo toka (TAMISEMI) alisema maeneo ya ukusanyaji kwa mashine (POS) ni Pamoja na kodi ya majengo.
Kiongozi huyo anayeongoza kamati yay a ulinzi na usalama wilaya aliwataka watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kutokaa maeneo yao ya kazi ambako wananchi wanawategemea wamwakilishe Rais Dkt. JohnPombe Magufuli kusikiliza kero zao na kuwatatulia.
Aidha Sanga aliweka bayana pongezi za Rais kwa kufanikisha ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita ingawa hajafurahishwa kwenye eneo la ukusanyaji mapato, usimamizi wa pesa na matumizi mabaya ya pesa mfano ujenzi wa miradi chini ya kiwango.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.