Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh.Filberto Sanga leo amekabidhi kiasi cha Tshs 92,084,500 kwa Vikundi 40 vya ujasiriamali vya wanawake na Vijana ambapo vikundi vya wanawake ni 16 na Vijana 24.
Akizungumza mbele ya vikundi hivyo Mh Sanga aliwataka wana vikundi kutumia fedha waliyopata kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo.
Sanga aliongeza kwa kusema" huu ni utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya awamu ya tano juu ya uwezeshaji kiuchumi kwa kuwakopesha vikundi vya wanawake na Vijana kwa asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Eng.Mshamu Munde alisema serikali kupitia Halmashauri imedhamiria kuwawezesha vikundi vya Vijana na wanawake kwa kuwakopesha kwa asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Munde aliongeza kwa kusema"hizi fedha sio zawadi mtumie kadiri mlivyoomba na mrejeshe vizuri ili muweze kukopa zaidi".
Halmashauri Wilaya Mkuranga kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 ilitenga Tshs 221,251,305 kwenye vyanzo vyake vya mapato ya ndani kwa ajili ya kukopesha vikundi vya kiuchumi vya wanawake na Vijana.
Aidha Halmashauri iliweza kutoa kiasi cha Tshs 199,200,000 kwa ajili ya kukopesha.Jumla ya vikundi 98 vya ujasiriamali vilikopeshwa kati ya hivyo vikundi 46 vya wanawake na 52 Vijana.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.