Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Waziri Kombo amewataka wajasiriamali kuhakikisha wanafanya marejesho ya mikopo yao kwa wakati.
Hayo ameyasema katika Mkutano wa mafunzo uliofanyika Agosti 12, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri alipokuwa akiongea na wajasiriamali hao.
Kombo amesema mikopo hii ya asilimia 10 siyo ya bure na kusisitiza kuwa kila kikundi kitakachopewa mikopo hii ya awamu ya robo ya nne ya Mwaka 2024/25 ni lazima irejeshwe kwa wakati ili iweze kuwanufaisha wajasiriamali wengine.
Aidha amewataka kuwa wazalendo katika matumizi ya mikopo hiyo na kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi ili kuweza kutumia fursa hii ya mikopo inayotolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mafunzo hayo ambayo yatadumu kwa muda wa siku tatu na kunufaisha jumla ya vikundi 76 yana lengo la kukumbushana namna ya kusimamia miradi, kuandaa kumbukumbu za shughuli za miradi ya kikundi pamoja na kuhakikisha wajumbe wanajua wajibu wao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.