Naibu waziri wa Afya Maendeleo Ya jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndungulile amesema Serikali inatarajia kuandaa mswada ambao utamtaka kila mwananchi kuwa na Bima ya afya ili kuepuka adha ya matibabu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zahanati ya kijiji cha Mkanoge Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Ndugulile alisema utaratibu huo unatarajia kuanza rasmi mwakani na wakati utakapofika bima ya afya haitakua hiyari tena.
Aidha amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kutoa taarifa wanapoona Dawa zilizo andikwa msd GOT kwani alama hiyo ni kuonesha dawa hizo ni mali ya umma na zikionekana kwa watu binafsi zinakua zimeibwa.
"Bajeti ya dawa imeongezeka mara dufu kutoka 30 bilion mwaka ulopita hadi 270 mwaka huu, nina simama kifua mbele kutangaza kua hatuna shida ya dawa" alisema.
Amewaahidi wanakijiji hao kuwa zahanati hiyo itafunguliwa akaunti bohari kuu ya dawa (msd) ili iweze kupatiwa dawa moja kwa moja ili kuboresha huduma.
Hata hivyo wananchi wameombwa kujiunga katika mfuko wa afya ambao utasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa jamii.
Mwanahawa Athuman alisema ufunguzi wa zahanati hiyo iliyo kamilika kwa milioni 100 itakua ni mwarobaini wa kudumu wa tatizo la afya kijijini hapo lililodumu kwa miongo kadhaa kwani Awali hakukua na huduma za afya na watu walilazimika kutembea umbali wa kilomita zaidi ya kumi kufuata huduma za afya.
Alisema wanawake walikuwa wanajifungua kwa njia za asili na baadhi hujifungua njiani wakielekea hospitali vijiji vya jirani.
Akizungumza katika ufunguzi huo Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbeto Sanga amewasihi wazazi kuhakikisha watoto waliofikisha umri wa kwenda shule waende ili kuwepo na wataalamu wa afya ambao ni wazawa.
Alisema wazazi wakihimiza watoto kusoma wilaya hiyo, kijiji hicho kitakua na wataalamu wa kutosha hivyo kumaliza tatizo la ukosefu wa wataalamu wa afya.
Pia amewaomba wananchi kutokuuza chakula chao badala yake kukihifadhi kwa matumizi ya badae kwani kwa kufanya hivyo nikujiweka katika hali mbaya ya uhitaji wa chakula.
"Ulinzi wa Wilaya yetu upo mikononi mwetu hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunadumisha ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa kuhusu wageni wanaofika bila taarifa au tunao watilia shaka, alisema.
"Kila mmoja wetu ni lazima kuhakikisha usalama na kipindi cha kuchekeana na kuvumiliana kimeshapita" aliongeza
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.