Wakazi wa Wilaya ya Mkuranga wametakiwa kuhamasishana kwenye kampeni kabambe ya kutokomeza mifuko ya plastiki ili kuepuka athari za kiafya na kimazingira.
Akizungumza na Wananchi wa wilaya hiyo kwenye kilele cha siku ya mazingira Duniani iliyofanyika leo kwenye kijiji cha Mwanambaya, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Juma Abeid alitaja athari za muda mrefu ni pamoja na kutooza kwa zaidi ya miaka (500)
Akifafanua zaidi Juma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magawa alisema kutooza huko kunaziba miundombinu ya majitaka na mifereji ya mvua na kuchangia mafuriko kuharibu ekolojia na bioanuai, vifo vya mifugo na viumbe wa baharini wanapokula.
Afisa Mazingira Wilaya, Herman Basisi katika Risala yake alisema wao tangu juni mosi hadi nne wamekua wakihamasisha jamii kwa kufanya mikutano ya hadhara sambamba na kuzunguka na gari la matangazo vijijini kuhimiza usafi wa mazingira maeneo ya viwanda, makazi na taasisi mbalimbali za serikali.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde, aliwaagiza wataalam na Viongozi kwenye vijiji na kata kuwaelimisha wananchi ili wakabidhi mifuko kwenye Ofisi zao huku akiahidi kufuatilia kwa kina viwandani na wauzaji waweke bei isiyowaumiza wananchi hatimaye wamudu kununua.
Akitoa neno la shukrani Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Diwani wa kata mwenyeji, Mipeko, Athumani Manicho alishindwa kutafuna maneno na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya na serikali kuu chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kufuatilia upendeleo kwao miradi sekta ya elimu afya, maji na miundombinu kwenye vitongoji mbalimbali
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.