Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga ikishirikiana na shirika la misaada ya kijamii (JSI) imekabidhi Baiskeli 11 na Makabati 11 kwa wasimamizi wa mashauri ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ngazi ya kata.
Vitendea kazi hivyo vimekabidhiwa na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Peter Nambunga kwa wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya kata ambao ni maafisa maendeleo ya jamii na maafisa ustawi wa jamii ngazi ya Kata.
Katika makabidhiano hayo, Nambunga amewataka maafisa hao kuzitumia baiskeli hizo pamoja na makabati (Cabinets) vizuri na kwa kazi zilizokusudiwa ili ziweze kudumu muda mrefu na kuleta tija kwa lile lililokusudiwa. Pia aliwashukuru wafadhili hao JSI na kuwaahidi kuwa halmashauri itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha kuwa tunafanya mapinduzi makubwa katika kuimarisha ulinzi na ustawi wa mtoto wa Mkuranga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.