Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imeaadhimisha wiki ya kilele cha Kichaa cha mbwa katika ofisi ya Kijiji cha Mkuranga Kata ya Mkuranga.
Katika maadhimisho hayo maafisa mifugo wa Wilaya waliweza kutoa huduma ya chanjo ya kichaa cha mbwa,dawa za minyoo na tiba pamoja na kuwapa huduma ya uogeshaji kwa mbwa.
Johnson J.Makalanga Afisa Tarafa Mkamba ambae ni kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga amewapongoza wananchi wa wilaya ya Mkuranga kwa kuweza kujitokeza kuwaleta mbwa kwaajili ya kupata chanjo kwani huwaepushia maradhi ikiwemo ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwani ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi na huambukizwa kwa njia ya kug'atwa na mbwa/paka/mnyama pori mwenywe ugonjwa huo.Binadamu pai kuambukizwa kwa kugusa mate ya mbwa mwenye kichaa.
Nae Bi.Anna Kiria Afisa kilimo,mifugo na uvuvi amesema Wilaya ya Mkuranga ina idadi ya Mbwa 2,453 na paka 963.Mbwa 1,785 na paka 132 walipatiwa chanjo dhidi ya kichaa cha Mbwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Aidha jumla ya kesi 71 za watu kung'atwa na mbwa ziliripotiwa katika ofisi ya Mkurugenzi kwa mwaka 2021/2022.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.