Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe Selemani Jafo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kufanya ujenzi wa shule mpya katika eneo la kipala mpakani ambalo lipo jirani na shule ya msingi Mwandege, sambamba na kukamilisha shule mpya ya Chatembo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya msingi Mwandege.
Mh Jafo alifikia uamuzi huo hapo jana baada ya kutembelea katika shule ya msingi Mwandege ambayo ina wanafunzi zaidi ya 3700 ambapo kati yao kuna ziaidi ya wanafunzi 560 ambao ni darasa la kwanza pekee.
Jafo alisema msongamano wa wanafunzi shuleni hapo umesababishwa na muitikio mkubwa wa elimu bila malipo ambapo wazazi wamehamasika kuwapeleka watoto wao kupata elimu.
Akizungumza mbele ya waalimu na wanafunzi wa shule hiyo Jafo amewaahidi kupeleka fedha ndani ya wiki hii kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa ili kupunguza kero ya mlundikano wa wanafunzi shuleni hapo.
“Ifikapo machi 06, mwaka huu vyumba vya madarasa viwe vimekamilika ili kupunguza idadi kubwa wa wanafunzi” Jafo alisema.
Katika ziara hiyo, Jafo amewaomba wananchi wa wilaya ya Mkuranga wamuunge mkono Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe Abdallah Ulega kwani anahangaika na kujituma sana kwa ajili ya kuwaletea maendelea wananchi wa Mkuranga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.