Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga ameishukuru na kuipongeza taasisi ya ‘Lions Club International’ kwa kazi kubwa zinazofanywa na taasisi hiyo kwa kujitolea kutoa huduma ya matibabu mbali mbali bure kwa wakazi wa Mkuranga
Sanga ameyasema hayo akifungua zoezi la utoaji wa huduma ya upimaji wa macho kwa wakazi wa Mkuranga zoezi ambalo limefanyika katika Hospitali ya wilaya ya Mkuranga ambapo pamoja na kutolewa huduma hiyo ya macho taasisi hiyo pia imefanikiwa kuwapima wakazi hao magonjwa ya sukari, shinikizo ladamu na utapia mlo kwa watoto na watu wazima.
Pamoja na hayo mkuu wa wilaya pia aliwashukuru kwa kutoa dawa bure na miwani kwa watu watakaogundulika na matatizo hayo na kuwataka kuendelea na moyo huo na kuwaomba wadau wengine kuiga mfano huo huku akiwataka kuongeza muda zaidi wa kutoa huduma hiyo sambamba na kuwataka wananchi kuwapa taarifa wenzao wanakoishi ili nao waweze kupata matibabu hayo kutoka katika taasisi hiyo ya lions club International.
Aidha Sanga amesema kwa mkuranga maeneo yapo mengi hivyo club hiyo wajiandae na kuja kupanga ni maeneo gani ewataona yanawafaa kwa ajili ya kujenga miundo mbinu mbalimbali itakayokuwa msaada kwa wananchi wa Mkuranga ikiwamo kituo cha afya na viwanja vya michezo
Kwa upande wake mkuu wa club hiyo kwa bara la Afrika Sayed Rizwan, alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwakaribisha na akaonesha kuridhika kwake na muitikio wa wananchi wa mkuranga, pia akaahidi zoezi hilo litakua endelevu huku akiahidi kutoa dawa na miwani bure kwa wote watakaogundulika na matatizo mbalimbali na wale watakaohitajika tiba zaidi nje ya wilaya club hiyo itagharamia kila kitu kwa huduma huduma hiyo.
Katika zoezi lililofanyia katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Lions Club International ikishirikiana na clubs nyingine nane wamefanikiwa kutoa huduma ya Macho, Kisukari, Shinikizo la damu na hali ya Lishe kwa watoto na watu wazima.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.