Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani amewataka wajasiliamali wanaojisughulisha na ufugaji wa kuku wa kisasa kueneza elimu wanayoipata kwenye mafunzo ambayo yanatolewa na wakufunzi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Wakala wa vyuo vya mafunzo na mifugo-LITA) yaliyofanyika leo katika ukumbi uliopo katika ofisi za Mkuu wa Wilaya Mkuranga
“Natoa shukrani kubwa kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, jambo la utoaji wa mafunzo ya ufugaji wa kuku ni jambo kubwa na nadhani mnatambua ni jambo la gharama sana, ukiona Serikali inagharamia jambo ni kwa kuwa lina umuhimu wake katika ustawi wa wananchi waliokusudiwa hivyo muwe mabalozi katika kusambaza Elimu mnayoipata hapa ili iwe na tija kwa wananchi wote ili kuweza kuyafanya maisha yetu kuwa bora lakini pia kupata kipato cha kijikimu na kufanya maendeleo yaayoonekana kwenye jamii” alisema..
Aidha Mhandisi Munde alitoa pongezi kwa Naibu waziri na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega kwa kueleza wazi kuwa Mbunge amekuwa mstari wa mbele sana kuhakikisha wananchi waliompa dhamana ya kuwaongoza wanafanya shughuli zinazowaingizia kipato na hivyo kupitia wizara anayoifanyia kazi amekua akishirikiana na wakufunzi kuwataka kuja mara kwa mara kutoa elimu kwa wananchi wa Mkuranga juu ya ufugaji wa kuku kwa njia bora na za kisasa ili kuwawezesha kuinua kipato chao.
Naye Mkurugenzi wa Utafiti Mafunzo na Ugani kutoka wizara ya mifugo na uvuvi, Dr. Angello Mwilawa alisema anawashukuru sana kwa kutekeleza mambo makubwa yanayohusiana na sekta ya mifugo na uvuvi katika tasnia mbali mbali lakini kuhusiana na nyama, mayai na upande wa samaki na ushahidi umekuwepo
Mwilawa aliongezea kwa kusema wizara ya mifugo na uvuvi imekua ikihamasisha ufugaji bora kwa wafugaji mbali mbali nchi nzima na hivyo kila sehemu kumekua na mikakati mbali mbali ya kuwezesha kufikia malengo waliojiwekea , hivyo kwa upande wa Mkuranga sehemu ya malengo ni pamoja na kutoa elimu mara kwa mara ili kuwajengea uwezo na hatimaye kufanikisha lengo la kuwa na wafugaji wa kisasa ambao watakua wanazalisha mifugo ambayo itakua na tija kwenye soko na hatimaye kupata kipato ambacho kitasaidia kuleta maendeleo mbali mbali kuanzia ngazi ya familia mpaka Nchi kwa ujumla wake..
Nyanza Mshoke, mmoja kati ya wanakikundi waliohuduria kwenye mafunzo hayo alisema anawashukuru sana Mh. Mbunge Jimbo la Mkuranga, Mkurugenzi Mtendaji ambaye ndiye msimamizi wa miradi ya maendeleo na wakufunzi wote kutoka wizarani kwa kutoa elimu bila kuchoka tena kwa nyakati tofauti.
“Wananchi wa Wilaya ya Mkuranga si wafugaji wa ngombe, mbuzi wala kondoo, isipokua kuku hivyo nafikiri hii ni sehemu pekee Mh Mbunge ametufanyia kuanzia sasa watendaji wa Wizara na Mh. Mbunge mjikite kutusaidia kwenye ufugaji wa kuku, mtupe elimu ya kutosha ili tutoke kwenye mawazo ya kuku ishirini tuliozoea kufuga kufikia kiasi cha kufuga kuku wengi ambao watatumika kama kitoweo kwenye familia, lakini watatumika kama sehemu ya kujiingizia kipato kitakachotumika kuleta aendeleo katika familia zetu” alisema.
Mafunzo haya yanatarajiwa kufanyika kwa mda wa siku mbili na takribani jumla ya vifaranga vya kuku 1200 vinatarajiwa kugaiwa katika vikundi mbali mbali vilivyo hudhuria mafunzo hayo …
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.