Katika kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini Mbunge wa Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi Mhe. Abdalah Ulega amewezesha kupatikana jumla ya pikipiki 45 kwa umoja wa vijana wa kikundi cha ‘Mkuranga Kwanza 2018’ wilayani hapa.Akikabidhi pikipiki hizo kwa vijana hao kwa niaba ya Mbunge huyo, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filberto sanga aliwataka vijana hao kuhakikisha wanazitumia pikipiki hizo maarufu kama Bodaboda kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo. “siku zote huwezi kufanya mambo yakafurahisha watu wote , kuna watu walikuja kwa lengo la kujaribu na wale waliokuja kwa nia njema na wale wote waliokua na mashaka nadhani sasa wote mmeshuhudia kwamba haikua ahadi hewa” alisema mkuu huyo wa Wilaya Pikipiki hizo zimetolewa kwa mkopo nafuu kwa vijana hao, ikiwa ni juhudi za mbunge wa jimbo hilo kushirikiana na benki ya Equity waliotoa mkopo kwa vijana hao pamoja na mzalishaji wa pikipiki hizo aina ya HAOJOE na SANLG kiwanda kilichopo eneo la kisemvule wilayani hapa.“Vijana hao wamepewa mkopo wa riba nafuu hii ni baada mbunge kubaini vijana hao walikua wanakopeshwa pikipiki kwa muda wa miezi 12 na anatakiwa afanye rejesho la Tsh10,000/= kila siku ambayo ni sawa na Tsh.3, 600,000/= kwa mwaka, ndipo mheshimiwa mbunge akaona atoe fursa hiyo ambaya jumla ya marejesho inafikia bei ya kiwanda kiasi cha Tsh2, 150,000/= tu” alisema Katibu wa Mbunge huyo Bwana Omary Kissatu akimuwakilisha Mbunge huyoWadau wa maendeleo waliyani haapo walipongeza juhudi za mbunge huyo na kuwaasa vijana hao kutumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi “tuna wabunge zaidi ya 300 nchii nzima,l,akini ukifanya utafiti utagundua ni wabunge wachache wanaowakumbuka kwa vitendo wapiga kura wao, na mmoja wapo ni mheshimiwa Abadalah Hamis Ulega” Alisema Muhidin Abdalah Diwani wa MkurangaKwa upande wake kamanda wa Polisi Wilaya ya Mkuranga (OCD) John Marro, mbali na kupongeza jitihada hizo aliwataka vijana hao kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani. Huku wanufaika wa msaada huo Abdalah Ninda na Ally Maega wakiongea baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo walipongeza suala hilo na kumtaka mbunge huyo kuwatafutia fursa zaidi ili waendelee kupiga hatua zaidi za kimaendeleo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.