Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Mhandisi Mshamu Munde 8/7/2020 asubuhi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya watu wa Indonesia Nchini Tanzania Prof. Dr. Ratlan Pardede, katika mazungumzo wamekubaliana kushirikiana katika kuendeleza na kudumisha ushirikiano wa kibiashara. Balozi wa Indonesia amesema yupo tayari kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Mkuranga na ameahidi kuanza ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kinatengeneza sabuni na losheni, mapema Januari 2021
Mhandisi Mshamu Munde amemuomba Balozi kuwashawishi wafanyabiashara na wawekezaji kuja Tanzania hususani Wilaya ya Mkuranga kwa ajili ya kuwekeza na kufanya biashara.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.