Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imefanya mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGOs ambao umefanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya.
Lengo la Mkutano ni kupeana uelewa wa pamoja katika nyanja ya NGOs,kubaini michango ya NGOs katika maendeleo ya Wilaya yetu ya Mkuranga,kubainisha changamoto na kuimarisha mahusiano kati ya Serikali ya Wilaya ya Mkuranga na NGOs zinazotoa huduma katika Wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali ambae ndie mgeni rasmi amesema Serikali haiwezi kufanya kila kitu ndio maana ikawaza kutunga sheria ya kuweza kuwaalika wadau ambao wapo njee ya serikali kuweza kuungana kuwasaidia wananchi wenye mahitaji.
Aidha ameyataka mashirika ya NGOs kuweza kujituma kwa bidii,kushirikiana na kutumia muda kujitafakari mengi ambayo yapo kwenye malengo yetu tukiweza kufanya hayo tutabadilisha taswira na matazamo na kuondosha changamato zilizopo ndani ya jamii zetu.
Nae Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantum Mgonja amesikitishwa kwa kuona NGOs zimeshindwa kuleta taarifa za kila robo katika Halmashauri ambazo zipo kwa mujibu wa sheria,kanuni.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.