Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Waziri Kombo ameagiza maafisa bajeti wote Wilayani humo kuhakikisha wanatumia mfumo wa manunuzi ya umma (Nest) ili kuweza kutekeleza takwa la kisheria la kufanya manunuzi kupitia mfumo huo.
Agizo hilo amelitoa leo akiwa katika Mkutano wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa manunuzi ya Umma (Nest) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwinyi Sekondari.
Aidha Mafunzo hayo yanayotarajiwa kufanyika kwa siku mbili yanaendeshwa na Kitengo cha Manunuzi kikishirikiana na wataalam wa Kitengo cha Tehama.
Mafunzo hayo yanatolewa kwa walimu na wakuu wa shule za msingi na sekondari, waganga wafawidhi pamoja na baadhi ya watendaji wa vijiji na wakuu wa Idara na vitengo wanaotekeleza miradi kwa sasa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.