Viongozi Wateule wa vyama vya mpira wa Netboli (Netball) na Mpira wa mikono (Handball) Wilaya ya Mkuranga wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu ili kuiletea sifa wilaya katika sekta ya michezo.
Hayo yamesemwa na Afisa Michezo wa wilaya hiyo, Ndugu Pembe Mlekwa, wakati wa uchaguzi wa kuwapata viongozi watakaongoza michezo hiyo ngazi ya wilaya, uliyofanyika juzi jumamosi katika ukumbi wa Resources Centre kiguza wilayani hapa.
Katika mkutano huo, ulishuhudia wajumbe wakiwachagua kwa kishindo Ndg. Rajabu Tuppa kuwa Mwenyekiti chama cha ‘Handball’ na Bi. Rhoda Chale kuwa Mwenyekiti chama cha ‘Netball’, pia walitumia haki hiyo ya kidemokrasia kuwapata makatibu wa vyama hivyo, waweka hazina pamoja na wajumbe mbalimbali
Kwa upande wao Viongozi hao wateule waliahidi kuleta mabadiliko chanya katika michezo hiyo na kuomba ushirikiano kutoka kwa wadau wengine ili kuitangaza Wilaya ya Mkuranga kitaifa
“Binafsi naahidi kuhamasisha mchezo huu wa ‘handball’ kuchezwa kuanzia shule za msingi mpaka sekondari na kwa kusaidiana na viongozi wenzangu naamini tutafika mbali” alisema Rajab Tuppa ambaye pia ni mwalimu wa michezo shule ya msingi Mpafu.
Nao wajumbe wengine, Ezra Kilomoni toka shule ya msingi Kerekese na Bi. Sofia Mgonja toka shule ya sekondari Mwarusembe, wakiongea kwa niaba ya wajumbe wengine walionesha kuridhishwa na uchaguzi huo na kutoa wito kwa viongozi hao kufanya kazi kwa umoja ili kuhakikisha sekta ya michezo hiyo inafanya vizuri
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.