Watendaji wa kata zote (25) Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani wametakiwa kuacha ofisi na kuwahi,miza watendaji wa vijiji washirikiane na wenyeviti wao kuitisha mkutano mkuu maalum utakaoeleza madhara ya DENGUE
Akizungumza kwenye kikao kilichoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Juma Abeid aliagiza vikao hivyo vifanyike haraka ili kuepukana na madhara zaidi
Aidha Diwani huyo wa kata ya Magawa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mhandisi Mshamu Munde kuhakikisha wataalamu idara ya afya waende kwenye vitongoji kutoa elimu sambamba na kushiriki mikutano mikuu maalum.
Kwa upande wake kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dk. Yeredi Chacha alitaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni homa kali, kuumwa kichwa ,viungo vya mwili sambamba na kutapika pia kutoka damu sehemu mbali mbali.
NayeAfisa Afya Wilaya Angelus Mtewa alizitaja kinga za ugonjwa huo ambao hauna dawa kuwa ni kufukia madimbwi ya maji, kunyunyuzia dawa kuua viluwiluwi kufyeka nyasi na vichaka karibu na makazi sambamba na kufunika mashimo ya maji taka kwa mfuniko pia kusafisha mitaro na gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama
Kikao hicho kilichohudhuriwa na madiwani wakuu wa dara . maafisa tarafa na wataalamu kilipokea taarifa ya uwepo wagonjwa (38) huku wakiazimia kuitishwa Baraza la kazi mapema ili kuzungumzia changamoto mbali mbali ikiwemo ugonjwa huo wa mlipuko.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.