Mkuu wa Wailaya ya mkuranga Mkoa wa Pwani Khadija Nasri Ali amempongeza Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto sugu ya ujenzi wa Barabara ya Lami kwenda Bandari Kongwe Kisiju kwa kuwaletea Pesa za Kujenga Kilometa 11.
Ameyasema hayo akiwa katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Miteza Wilayani Mkuranga na kutoa shukrani kwa viongozi mbalimbali ndani ya Wilaya hiyo bila ya kumsahau Mh. Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega
Aidha kiongozi huyo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliweka bayana pongezi kwa Marais Wastaafu kwa kuwatoa kwenye mnyororo wa ukandamizaji na kudumisha amani na utulivu ambao ni msingi wa Maendeleo sambamba na kuweka wazi uboreshaji wa sekta ya Elimu ambayo inawafanya vijana wapate ajira mbalimbali viwandani.
Akitoa ushuhuda wa Mwasisi wa CCM na serikali ya Hayati Mwl. Nyerere Mzee Maarufu Kijiji cha Miteza Kata ya Njia nne aliweka bayana Hayati alifanya ziara wilayani Mkuranga kutembelea vijiji 42 zamani wakiwa Wilaya ya Kisaraweakianzi Kijiji chao Wazee maarufu akiwemo Mzee huyo wkamwomba sehemu ya eneo la wekezaji Habibu kupitia Baba wa Taifa akawapa wakajenga Shule ya Msingi ambayo hadi leo ipo.
Akitoa salamu za HAlmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mwantum Mgonja amesema wametoa mikopo ya wajasiriamali milioni 220 na katika Sekya ya Elimu amempongeza Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea Kiasi cha Shilingi Bilioni 2.64 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa 132 yatakayowezesha kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Mwakani.
Kauli mbiu ya Mwaka huu katika kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru ni “Amani na Umoja ni Nguzo ya maendeleo yetu”.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.