Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amezitaka taasisi wezeshi kushiriki moja kwa moja kwenye mbio za mwenge.
Hayo ameyasema leo Wilayani Mkuranga wakati wa Ziara ya ukaguzi wa Miradi itakayopitiwa na Mwenge maalum wa Uhuru ifikapo Agosti 16, 2021
Aidha Mkuu huyo amesisitiza kuwepo kwa nyaraka muhimu zinazo fafanua gharama halisi za mradi, namna malipo yalivyofanyika na mikataba ya ujenzi wa miradi ili kuepuka ukosefu wa maksi usio wa lazima.
Akiendelea, amewataka waratibu wa mwenge wilaya kuhakikisha itifaki ya mwenge inazingatiwa na pia ukaguzi wa magari yote yatakayotumika siku ya mapokezi ya mwenge unafanyika chini ya jeshi la polisi ili kuhakikisha uimara na ubora wa magari hayo.
Akizungumza wakati wa Majumuisho Mhe. Kunenge alimpongeza Mkuu wa Wilaya Mhe. Hafija Ali na Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Mshamu Munde kwa kusimamia vyema ujenzi wa miundo Mbinu na uratibu wa miradi yote ambayo imewezesha ziara yake ya ukaguzi kuwa nyepesi.
Miradi iliyokaguliwa ni skimu ya maji katika kijiji cha mkerezange, zahanati ya Mwarusembe, bwalo la chakula mwinyi sekondari.
Miradi mingine ni pamoja na Mradi wa maji endelevu katika kijiji cha Mwanambaya na kiwanda cha kuzalisha nyaya za fiber, miradi yote inakadiliwa kuwa na thamani ya takribani kiasi cha shilingi bil. 21
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.