Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakar Kunenge amewataka Wakuu wa wilaya za Mkoani Pwani kutumia wazo la Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri Ally la kuanzisha matamasha ya utalii kama njia moja wapo ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyomo katika maeneo yao.
Mh Alhaji Kunenge ambaye aliongoza mamia ya wakazi wa Mkuranga na maeneo mengine nchini walioshiriki tamasha hilo ili kujionea vivutio vya utalii vilivyopo katika msitu wa vikindu alisema vivutio vilivyomo ndani ya msitu huo kama vitatangazwa vitavutia watu wengi kutalii katika msitu huo.
Alisema uanzishwaji wa tamasha hilo si kwamba linakwenda kutangaza vivutio vya utalii vya wilayani mkuranga lakini pia ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kutaka kutangaza kimataifa vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini
Alisema Mkoa wa Pwani umejaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ikiwemo ,historia za kikoloni, fukwe za bahari na hata hifadhi za misitu ambazo ndani yake kuna vivutio vingi vya utalii na kwamba vikitangazwa vyema vinaweza kuufanya mkoa wa Pwani kuwa kitivo cha utali hapa nchini Tamasha hilo limeambatana na burudani mbalimbali za mbio ndefu na fupi, burudani yak muziki, kuvutana Kamba na shindano la wanawake na wanaume kukuna nazi ambapo washindi walipewa zawadi na medali za shaba
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.