Wananchi wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wametakiwa kuyatumia mafunzo ya ufugaji wa kisasa hatimaye wajikwamue kiuchumi sambamba na kupaisha mapato ya Halmashauri ya Wilaya
Akifungua mafunzo ya wafugaji wa Wilaya hiyo kwenye ukumbi wa Flex Hotel leo, gNaibu Waziri wa mifugo na uvuvi Abdalla Ulega aliwataka washiriki wawe wasikivu na kuwa mabalozi kwenye vitongoji hadi vijiji
Aidha Ulega alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Luhaga Mpina kwa kuichagua wilaya hiyo ambayo yeye ni Mbunge kutoa elimu ya ufugaji bora
Aidha ulega amewataka wananchi wajikite kwenye ufugaji kama mbadala wa kilimo cha korosho , huku akishukuru wizara kwa kuichagua wilaya hiyo kuwa kituo cha uksanyaji maziwa kwa kanda sambamba na kiwanda cha chakula cha mifugo ambacho malighafi yake ni mihogo
Mbunge huyo wa jimbo la Mkuranga alitaja fursa nyingine ni ujio wa Benki ya kilimo ambayo itakopesha vikundi vya wafugaji na wavuvi kwa masharti nafuu
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde alishukuru ujio wa wataalamu toa wizarani huku akiweka bayana viwango ardhi ya kutosha kwa ajili ya viwanda mbalimbali vinavyotoa fursa kwa wakulima na ufugaji
Akizungumza wakati wakufunga mafunzo hayo mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbeto Sanga alisema anaishukuru wizara kwa kuleta mafunzo hayo kwani inawezekana ikawa muorobaini wa wafugaji kahamahama na kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji katika wilaya hiyo .
Aidha aliwataka washiriki wawe na utayari kwani soko la uhakika la kuuza maziwa, nyama na mihogo lipo tayari
Akimalizia aliiomba serikali iwafikirie kuwapa msitu wa masanganya ambao utakuwa tiba katika migogoro ya wafugaji na wakulima
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.