WADAU WA ELIMU MKURANGA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUENDELEZA ELIMU BURE
Rais Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kuendelea kusimamia sera ya elimu bila malipo hali inayochangia ongezeko la wanafunzi ngazi mbali mbali wakiwemo wasio na uwezo kiuchumi
Akifungua kikao cha wadau wa maendeleo kwenye sekta ya elimu Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani jana mwenyekiti wa kikao ambaye pia Mkuu wa Wilaya Khadija Ally aliweka bayana mafanikio kupitia mkakati huo wa serikali ya awamu ya tano na sita wamepokea sh. Bl.1. 697,259 kwa sekondari na bil. 2.316y,261 kwa msingi kuanzia mwaka 2018-2019 hadi 2020/21.
Mkuu huyo aliwaomba wadau wakiwemo wahisani kuweka nguvu zao wakishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ili kutekeleza maagizo ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (TAMISEMI) Ummy Mwalimu kwa kujenga miundo mbinu ya madarasa, vyoo, nyumba za walimu sambamba na madawati ili wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza , elimu ya wali na msingi wawe madarasani kwa mkupuo.
Khadija ambaye pia anaongoza kamati ya ulinzi na usalama aliagiza kukomeshwa mmomonyoko wa maadili sambamba na kuwachukulia hatua za kisheri awanaowapa ujauzito wanafunzi.
Akitoa taarifa ya hali ya elimu Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye pia ni katibu wa kikao Mwantumu Mgonja alizitaja baadhi ya changamoto ni uwepo wa ongezeko kubwa a wanafunzi unachangia mahitaji makubwa ya miundombinu , walimu na madawati.
Akitoa salaam zake Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega alimpongeza Rais kwa kazi kubwa ya kujenga madarasa vijijini huku akiahidi kushirikiana na (SIDO) na (VETA) ili kila Kijiji na kata pawepo karakana ili vijana wapate ajira kutengeneza na kukarabati madawati huku Jukwaa la wanawake watengenezesare za wananfunzi nayo Halmashauri ya Wilaya ijikite kupika chakula ili kupunguza utoro na kuongeza ufaulu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.