LSP (local service provider) wasimamizi wa mradi ngazi ya jamii wamepewa mafunzo ya kujua wajibu wa majukumu katika miradi itakayotekelezwa na walengwa.
LSP watakuwa na jukumu la kuwasimamia walengwa jinsi ya kutekeleza miradi ambayo inatakiwa kutekelezwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ina miradi 122 ambayo itatekelezwa na walengwa kutoka katika Kaya hizo ni miradi ambayo itakuwa na viwango katika sekta mbalimbali na ubora.
Usimamizi wa miradi hii iliyoibuliwa na walengwa itatekelezwa kwa kipindi cha Mwaka 1 ni ajira za muda mfupi ambapo utekelezaji wake unategemea nguvu kazi za walengwa wenye umri kuanzia miaka 18 - 65 watabuni miradi itakayosaidia jamii zao na baada ya utekelezaji miradi hii itasimamiwa na serikali ya vijiji vyao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.