Waandishi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wilaya ya mkuranga Mkoa wa Pwani wametakiwa kutekeleza kwa vitendo viapo vyao kwa kutotoa siri huku sheria ikichukua mkondo wake.
Akizungumza nao baada ya kiapo Msimamizi mkuu wa uchaguzi wilayani humo Hassani Njama alisema dhima ya nchi ya kuwaweka viongozi wa Serikali za Mitaa madarakani ipo mikononi mwao.
Aidha njama alitumia fursa hiyo kuvitangaza vituo vya Mkuranga,kisiju, na Kimanzichana ambavyo vitaendesha mafunzo maalumu ya siku mbili kuanzia juzi yatakayoshirikisha wasimamizi wasaidizi ngazi ya vijiji, kata na wilaya sambamba na waandikishaji ambao jumla yao ni (600).
Kwa upande wake afisa uchaguzi Salumu Mwamfula aliwataka washirikishi wa mafunzo hayo kuhakikisha wanawahi mapema kwenye vituo vyao hatimaye mafunzo hayo yalete tija kwa Taifa.
Awali Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Mkuranga Kenneth Mrosso aliwapa kiapo wasimamizi wasaidizi huku wakiahidi kutekeleza maujukumu yao vizuri wakimtanguliza mwenyezi mungu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.