Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt Mary Mwanjelwa, amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kuzingatia Ueledi, Ubunifu na Kujituma ili kutimiza adhma ya serikali ya Awamu ya tano kuchapa kazi na kufikia uchumi wa kati
Akiyasema hayo katika mkutano maalum na watumishi wa Umma wa halmashauri ya wilaya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo, Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa Umma kuzingatia sheria, taratibu na kanuni katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha Mhe. Naibu Waziri akatumia fursa hiyo pia kuwaasa watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuwatahadharisha Wakuu wa Idara na Vitengo kuwa endapo watashindwa kuwasimamia watumishi waliochini yao watawajibika kwa mujibu wa sheria maana wamepewa dhamana ya kuwaongoza.
Akizungumza na watumishi ambao ni wasaidizi katika kada mbalimbali,Naibu waziri amewataka kuheshimu na kutekeleza maelekezo ya viongozi wao pasipo kusukumwa kwa mujibu wa sheria za Utumishi wa Umma.
Mwisho naibu Waziri amewataka watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kuwa wazalendo na waadilifu kwani serikali ya awamu ya tano chini Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ni ya uadilifu na si vinginevyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.