Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu leo amewahakikishia wawekezaji wa kiwanda cha Lodhia Group of Companies kuwa changamoto zinazowakabili za kukosa malighafi za kutengeneza bidhaa zinazotokana na chuma zinatatuliwa kwa wakati mara baaada ya kukaa na timu yake na kuweka mchanganuo wa jinsi ya kutatua changamoto hizo.
Akiongea katika ziara wakati alipotembelea kiwanda cha Lodhia alisema amepata taarifa za changamoto ya kukosa malighafi kutokana na matatizo ya kupanda kwa gharama za tozo kwa wauzaji wadogo wadogo wa chuma chakavu yanayoelekea kukwamisha upatikanaji wa vyuma chakavu ambavyo ndo malighafi pekee wanayotegemea katika utengenezaji wa bidhaa za chuma
“Lakini pamoja na yote nimefarijika sana kuona namna kiwanda kinavyofanya kazi vizuri pamoja na changamoto mnazokabiliana nazo mmekuwa wazalendo wa kulipa kodi za serikali kwa uaminifu mkubwa na hasa kwenye matumizi ya umeme mnalipa mpaka bilioni 6, kwa mantiki hii kiwanda kinaonekana kinafaya kazi vizuri hivyo sina budi kama serikali na muwakilishi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya jitihada za wazi na haraka za kutatua changamoto inayowakabli”
Akielezea changamoto zinazozikabili kiwanda hiko Mkurugenzi wa udhalishaji Ndg. Sculesh Pandit amesema uwezo wa tanuru yetu katika uzalishaji wa vyuma ni mkubwa kuliko malighafi ya chuma chakavu inayopatikana hapa nchini hivyo tunahitaji kuagiza malighafi ya chuma chakavu kutoka nje ya nchi kwani Tanuru ina uwezo wa kuzalisha tani 8000 kwa mwezi kwa hiyo tunahitaji tani 9000 kwa mwezi lakini tunapata tani 2000 kwa mwezi alisema.
Pandit alisisitiza kuwa uingizaji wa chuma chakavu kama malighafi ni muhimu kwa uhai wa viwanda vyetu hapa nchini ili kuzalisha billets zenye ubora wa hali ya juu hivyo basi tunaziomba mamlaka husika na serikali kurekebsha shera na kanuni na pia kupunguza urasimu usio wa lazima kwani chua chakavu inayopatikana hapa nchini ubora na viwango vya kutengeneza nondo aina TMT B500. (Thermo Mechanically Treated Steel)
Aidha Pandit alieleza madhara yanayotokana na changamoto za kiwanda kusimama ni pamoja na ukosefu wa ajira, mapato ya serikali kukosekana, na hivyo kupelekea mapato yanayotokana na kiwanda hiko kushuka
Pandit aliongeza kwa kusema kuwa Lodhia ni kiwanda cha kwanza Tanzania kinachozalisha nondo ya milimita 40 B-500 ambayo inatumika kwenye miradi mikubwa ya ujenzi kama mradi wa daraja la Salender na Nyerere Hydro Power.
Wakati akimalizia wasilisho la hotuba yake Pandit alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa kuanzisha sera ya Tanzania ya Viwanda , na ameomba taasisi zake ziwape ushirikiano wa karibu , kusikilizwa na kutatuliwa kwa changamoto zao kwa wakati.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.