Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2022 umetembelea Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na kukimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Miradi ya Maendeleo.
Mwenge wa Uhuru uliweza kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa vyumba vya madarasa, barabara sambamba na mradi wa maji
Pamoja na hilo viongozi wa mbio za mwenge waliweza kutembelea kikundi cha vijana kinachojihusisha na shughuli za uchongaji wa fenicha
Aidha, Mwenge wa Uhuru ulipokea taarifa ya utekelezaji wa masuala ya mtambuka ikiwemo masuala ya Ukimwi, muwasilishaji alisema wilaya imeendelea kutoa huduma kwa wanaoishi na Virusi vya ukimwi na upimaji wa hiari ambapo jumla ya watu 35316 wamepima kati yao 1695 sawa na asilimia 4.8 wamebainika kuwa na virusi vya ukimwi.
Nayo taarifa ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya iliweza Wilaya kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wameendelea kutoa elimu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya lwa jamii, ambapo jumla ya watu 269 wamefikiwa na waathirika 111 wanapata huduma na tiba.
Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Mkuranga umekimbizwa kilomita 149.50 katika kata 10 umezindua miradi miwili umeweka jiwe la msingi miradi mitatu na kuona miradi mitano mitatu ni ile ya jumbe za Mwenge kadhika ujumbe wa Mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2022 wenye kauli mbiu isemayo "SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO YA TAIFA SHIRIKI KUHESABIWA, TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA".
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.